Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu wa zamani wa Togo afariki akiwa uhamishoni

Waziri Mkuu Togoo.png Waziri Mkuu wa zamani wa Togo afariki akiwa uhamishoni

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasiasa wa upinzani wa Togo na Waziri Mkuu wa zamani Agbéyomé Kodjo, ambaye alishika nafasi ya pili katika uchaguzi wa rais wa mwka 2020, alifariki Jumapili akiwa uhamishoni akiwa na umri wa miaka 69, mmoja wa viongozi wa muungano wa vyama vya siasa ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatatu.

"Agbéyomé Kodjo alifariki siku ya Jumapili nchini Ghana, kufuatia kuugua," Thomas Kokou N'soukpoe, mmoja wa viongozi wa Dynamique Monseigneur Kpodzro (DMK), muungano wa vyama vya siasa uliomuunga mkono mwanasiasa huyo wa upinzani katika uchaguzi wa urais 2020, ameliambia shirika la habari la AFP.

Bw. Kodjo alipata 19.46% ya kura katika uchaguzi wa urais mnamo Februari 22, ikilinganishwa na 70.78% ya Faure Gnassingbé, kulingana na matokeo rasmi ambayo amekuwa akiyapinga kila wakati. Mnamo mwezi wa Julai 2020, mpinzani huyo alikimbilia Togo, kufuatia kuitishwa mahakama na waranti wa kimataifa wa kukamatwa dhidi yake.

Waziri Mkuu wa zamani mwanzoni mwa miaka ya 2000, Agbéyomé Kodjo alishikilia nyadhifa kadhaa za uwaziri chini ya Jenerali Gnassingbé Eyadéma ambaye alitawala Togo kwa mkono wa chuma kwa miaka 38.

Bw. Kodjo alifukuzwa kazi mwaka wa 2002 na kufungwa kwa miezi michache nchini Togo, kabla ya kujiunga na upinzani na kuunda mwaka 2008, chama chake cha OBUTS, ambacho mwaka 2018 likawa chama cha Wazalendo Demokrasia na Maendeleo (MPDD).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live