Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu wa zamani Burundi ashindwa rufaa, arejeshwa jela maisha

Bunyoni Burundi.jpeg Jenerali Alain Bunyoni

Sun, 30 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Burundi Jenerali Alain Guillaume Bunyoni ameshindwa katika rufaa yake baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha Gerezani.

Alain Guillaume Bunyoni ataendelea kutumikia kifungo cha maisha Gerezani, kulipa faini ya Bilioni 22 na milioni 713 na kukamatwa kwa mali zake ambazo hakuziweka hadharani mwaka wa 2021.

Bw. Bunyoni amekutwa na hatia ya makosa saba ikiwemo la kupanga njama za kutaka kumuua Rais wa Burundi Meja Jenerali Evariste Ndayishimiye, kupanga njama za Mapinduzi na kuhatarisha usalama wa nchini na kuhujumu uchumi.

Washukiwa wengine watatu ambao ni Kanali Desire Uwamahoro aliyekuwa Kiongozi wa Polisi wa kutuliza ghasia, Bapfumukeko Samuel Destino na Niyonsaba Côme wote wamehukumiwa kifungo cha miaka 15 Gerezani kwa kushirikiana na Alain Guillaume Bunyoni katika kutaka kutekeleza mipango yake.

Wakili wa Alain Guillaume Bunyoni, Placide Gatoto amesema kuwa wanakwenda kukata rufaa baada ya kutoridhishwa na hukumu hiyo iliyotolewa dhidi ya mteja wake.

Waziri huyo Mkuu wa zamani wa Burundi alikamatwa mwezi Aprili 2023, miezi sita baada ya kuondolewa katika wadhifa wake baada ya kuteuliwa mwaka wa 2020 na Rais Evariste kuhudumu katika nafasi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live