Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu wa Ethiopia amteua mkuu wa TPLF kama rais wa Tigray

Waziri Mkuu Wa Ethiopia Amteua Mkuu Wa TPLF Kama Rais Wa Tigray Waziri Mkuu wa Ethiopia amteua mkuu wa TPLF kama rais wa Tigray

Thu, 23 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amemteua mwanachama mwandamizi wa chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF) Getachew Reda kuwa mkuu wa utawala wa mpito ulioanzishwa katika eneo la kaskazini la Tigray.

TPLF, ambayo ilipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka miwili dhidi ya serikali ya shirikisho, ilimteua Bw Getachew wiki jana.

Maelfu ya watu walikufa katika mapigano hayo na mzozo huo ukazua mzozo mkubwa wa kibinadamu.

Pande zote zimeshutumiwa kutekeleza uhalifu wa kivita na utawala wa Marekani.

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya amani ambayo TPLF na serikali ya muunga walikuwa wametia saini nchini Afrika Kusini.

Utawala wa muda wa jimbo hilo utakuwa katika nafasi yake hadi uchaguzi wa kikanda ufanyike chini ya usimamizi wa tume ya uchaguzi.Tarehe bado haijawekwa.

Baraza la wawakilishi wa Watu wa Ethiopia hapo jana Jumatano liliondoa TPLF katika orodha ya magaidi.

Chanzo: Bbc