Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu wa Burundi atupwa jela maisha

Bunyoni Burundi.jpeg Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Burundi, Alain-Guillaume Bunyoni.

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Juu nchini Burundi imemuhukumu kifungo cha maisha jela Waziri Mkuu aliyeondolewa madarakani Alain-Guillaume Bunyoni siku ya Ijumaa kwa tuhuma za kujaribu kupindua serikali na kutishia maisha ya Rais.

Bunyoni, ambaye kesi yake ilifunguliwa miezi mitatu iliyopita, alikuwa Waziri Mkuu kuanzia mwaka 2020 hadi Septemba 2022 alipofutwa kazi, siku chache baada ya Rais Evariste Ndayishimiye kuonya kuhusu njama ya "mapinduzi" dhidi yake.

"Alihukumiwa kifungo cha maisha jela (kwa makosa)... ikiwa ni pamoja na kupanga njama dhidi ya mkuu wa nchi kupindua utawala wa kikatiba", chanzo cha mahakama kiliiambia AFP kwa sharti la kutotajwa jina.

Jenerali huyo wa jeshi pia alituhumiwa kutumia uchawi kutishia maisha ya mkuu wa nchi, kudhoofisha usalama wa taifa, kuyumbisha uchumi na kujitajirisha kinyume cha sheria.

Mahakama, ambayo ilikutana katika mji mkuu wa kisiasa wa Gitega, iliamuru mamlaka kutaifisha nyumba na majengo manne pamoja na sehemu ya ardhi na magari 14 ya Bunyoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live