Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu atangaza kiama na walioshambulia Tripoli

Tripoli Pm Waziri Mkuu atangaza kiama na walioshambulia Tripoli

Mon, 29 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Libya amesema, sheria itachukua mkondo wake dhidi ya kila aliyehusika na mashambulizi ya mjini mkuu wa nchi hiyo, Tripoli.

Shirika la habari la IRNA limemnukuu Abdul Hamid Al-Dabibah akisema hayo usiku wa kuamika leo Jumatatu ikiwa ni kujibu mapigano yaliyotokea juzi Jumamosi katika mji mkuu Tripoli na kusisitiza kuwa, serikali yake imeshachukua hatua mbalimbali za kuwafuatilia wahusika wa mapigano hayo na wote watapashindwa kizimbani na kuhukumiwa kwa kuhusika na machafuko hayo.

Waziri Mkuu huyo wa Serikali wa Umoja wa Kitaifa ya Libya GNU pia amesema, msiba na balaa tulilo nalo leo Libya ni kwamba baadhi yetu wameamua kufanya uhalifu na mashambulio ya kinyama dhidi ya mji mkuu Tripoli na wengine kufikia hata kuunga mkono mauaji na mashambulio hayo.

Jana Jumapili, duru za tiba nchini Libya ziliripoti kuwa watu wasiopungua 23 wameuawa na kwa uchache 87 wamejeruhiwa katika mapigano makali yaliyozuka upya Jumamosi asubuhi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli.

Taarifa iliyotolewa na mrengo wa GNU imesema mapigano hayo mapya yaliyozuka mjini Tripoli yalichochewa na hatua ya wapiganaji watiifu kwa mrengo wa Bashagha kuufyatulia risasi msafara wa askari wa serikali hiyo ya Umoja wa Kitaifa.

Kwa upande wake, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran, Nasser Kan'ani Chafi, ameelezea kusikitishwa sana na machafuko mapya ya nchini Libya na ametaka kukomeshwa mara moja mapigano hayo.

Amesema, Jamhuri ya Kiislamu inazitaka pande hasimu kuzingatia maslahi ya taifa, usalama wa wananchi na kutatua mambo yao kwa njia ya mazungumzo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live