Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu anatafutwa na polisi

Alain Guillaume Bunyoni Waziri Mkuu anatafutwa na polisi

Fri, 21 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka nchini Burundi zimeanzisha msako dhidi ya waziri mkuu wa zamani Alain-Guillaume Bunyoni, miezi saba tangu afutwe kazi.

Bunyoni, ambaye kwa wakati mmoja alikuwa mkuu wa polisi na waziri wa usalama, alifutwa kazi septemba mwaka jana, katika hatua ya mabadiliko ya kwanza makubwa tangu rais Evariste Ndayishimiye kuchukuwa madaraka 2020.

Inaripotiwa kuwa siku ya jumatatu polisi na maafisa wa upelelezi walifanya msako katika makaazi yake matatu, lakini hawakufanikiwa kumpata, waziri wa usalama wa ndani Martin Niteretse akisema bado wanamtafuta Bunyoni.

Afisa mmoja wa juu wa jeshi ameiambia AFP kwamba, wamemkamata afisa mmoja wa polisi ambaye anadaiwa kumtaarifu Bunyoni kuhusu oparesheni ya kumsaka, hali iliomfanya kukimbia kabla ya maafisa wa polisi kufika.

Bunyoni, mtu mwenye ushawishi katika chama tawala cha CNDD-FDD na ambaye aliteuliwa waziri mkuu 2020 alifutwa kazi siku chache baada ya rais Ndayishimiye kuonya kuhusu mpango wa mapinduzi dhidi yake.

Ndayishimiye alichukua mamlaka mnamo Juni 2020 baada ya mtangulizi wake Pierre Nkurunziza kufariki kutokana na kile mamlaka ya Burundi ilisema ni changamoto za kupumua huku kukiwa na uvumi ulioenea kuwa aliaga dunia kutokana na Covid-19.

Amesifiwa na jumuiya ya kimataifa kwa kuaanza kuirejesha Burundi katika ulingo wa kimataifa ya kutengwa chini ya utawala wa Nkurunziza. Lakini ameshindwa kuboresha rekodi mbaya ya haki za binadamu na nchi yenye watu milioni 12 inasalia kuwa miongoni mwa nchi maskini zaidi duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live