Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu Sudan awekwa kizuizini na wasiojulikana

Pm Arreted Waziri Mkuu wa Sudani Abdallah Hamdok

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mapema Oktoba 25, 2021, imeripotiwa kuwa Waziri Mkuu wa Sudani Abdallah Hamdok aliwekwa kizuizini akiwa nyumbani kwake na vikosi vya kijeshi ambavyo hadi sasa havijafahamika ambavyo vilizingira makazi ya kiongozi huyo.

Taarifa hii imetolewa na kituo cha televisheni cha Al Hadath cha nchini humo ambacho pia hakikuweka bayana kuhusu wahusika wa tukio hilo.

Hadi saa inaelezwa kuwa Serikali pamoja na Jeshi la nchini humo hawajatoa tamko kuhusu tukio hilo linaopasua ngoma kitaifa na kimataifa.

Awali kabla ya tukio hilo jeshi la nchini humo lilimkamata afisa habari wa Waziri huyo.

Pia kikosi hicho kisichofahamika kimewashikilia mawaziri wengine wanne na mwanachama mmoja wa chama tawala cha Sovereign Council.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live