Sudan.Waziri Mkuu wa Sudan, Abdalla Hamdok amenusurika kifo baada ya msafara wake kushambuliwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum. Msafara huo umeshambuliwa leo Jumatatu Machi 09, 2020 wakati waziri mkuu akielekea ofisini kwake. Vyombo vya habari vya kimataifa vimeripoti kuwa maofisa kutoka katika ofisi yake wamethibitisha msafara huo kushambuliwa. Taarifa zinasema kuwa, waziri huyo mkuu ambaye aliingia madarakani mwezi Agosti mwaka jana yuko salama na amehamishiwa katika eneo salama. Bado hakuna taarifa za mtu au kikundi kuhusika na shambulio hilo. Picha zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha magari mawili meupe yaliyokuwa yanatumiwa na viongozi wenye nyadhifa za juu nchini humo yakiwa yameharibiwa na vioo vikiwa vimevunjika huku gari lingine likiwa limeharibiwa vibaya na mlipuko huo.