Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu Sudan aachiwa huru

Aachiwa Waziri Mkuu wa Sudani Abdallah Hamdok

Wed, 27 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok, amerudishwa nyumbani kwake Oktoba 26,2021 mara baada ya kuwepo kwa shinikizo kubwa la kimataifa la kutaka kuachiwa kwa kiongozi huyo mara baada ya kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika nchini humo.

Ofisi ya Waziri Mkuu imethibitisha kuachiwa kwa kiongozi huyo na kusema kuwa alikuwa chini ya uangalizi mkali na wa karibu huku mawaziri wengine wanne pamoja na raia mmoja wakiwa chini ya ulinzi mara baada ya jeshi kuvamia ofisi hiyo mapema Oktoba 25, 2021.

Siku ya tukio hilo Marekani na Umoja wa Nchi za Ulaya EU katika nyakati tofauti walilitaka jeshi hilo kumuachia Waziri huyo na kuwa wasipofanya hivyo basi watasitisha misaada ya moja kwa moja kwa jeshi hilo ambalo kwa sasa linaongoza nchi ya Sudan.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alitoa tamko kutaka Waziri Mkuu achiwe mara moja kauli ambayo iliambatana na kikao cha ghafla ya Kamati ya Ulinzi ya UN.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live