Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu Somalia athibitisha kuwepo kwa uchaguzi mkuu

Waziri Mkuu Somaliaaa Hussen Robel, Waziri Mkuu Somalia

Mon, 13 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu nchini Somalia, Hussein Robel amesema kuwa uchaguzi mkuu wa nchini humo utaendelea kama ulivyopangwa na Tume ya Uchaguzi licha kuwepo kwa sintofahamu baina ya Waziri huyo na Rais wa nchi hiyo Mohamed Abdullahi Mohamed.

Waziri huyo ameyasema haya wakati wa alipotembelea ofisi za wanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa, na kusisitiza kuwa mipango ya uchaguzi mkuu ipo palepale na kuwa tofauti hizo hazina mashiko.

Sintofahamu hiyo imekuja kufuatia kupishana kwa misimamo baina ya viongozi hao katika uteuzi wa Waziri wa ulinzi pamoja na Mkuu wa jeshi la Usalama la nchi hiyo, wakati taifa hilo likiwa mchakato wa kuandaa uchaguzi huo ambao umechelewa kufanyika kwa miezi kadhaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live