Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu Ethiopia atoa saa 72 kwa waasi

Mtanzanianews 127247286 202561701351109 5209629747512460002 N 660x400 Waziri Mkuu Ethiopia atoa saa 72 kwa waasi

Mon, 23 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, ametoa muda wa saa 72 kwa vikosi vya mkoa wa Tigray kujisalimisha kabla ya jeshi la shirikisho kuanza kuushambulia vikali mji mkuu wa Mekelle.

Waziri Mkuu Abiy ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, aliandika katika ukurasa wake wa Twitter akiwataka wapiganaji wa Tigray kujisalimisha kwa amani, wakitambua kuwa hakuna kurudi nyuma.

Mapema jana Jumapili, jeshi la Ethiopia lilitishia kuuzingira mji wa Mekelle unaokaliwa na maelfu ya raia. Msemaji wa jeshi la Ethiopia Dejene Tsegave amewaeleza wakaazi wa mji huo kujiokoa na kujiweka mbali na wanajeshi wa mkoa.

Hata hivyo kiongozi wa chama tawala cha Tigray TPLF, Debretsion Gebremichae ameahidi mapiganao makali kulizuia jeshi la shirikisho kusonga mbele.

NABII BUSHIRI, UTAJIRI WA KUTISHA, MALI KUSHIKILIWA, ANA NDEGE, JUMBA LA KIFAHARI, MAGARI

Chanzo: millardayo.com