Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu Ethiopia atangaza kuwa mstari wa mbele vita dhidi TPLF

Abiy Pic Waziri Mkuu Ethiopia atangaza kuwa mstari wa mbele vita dhidi TPLF

Tue, 14 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amerejea katika mstari wa mbele na kutangaza ushindi zaidi dhidi ya kundi la Tigray People’s Liberation Front (TPLF).

Katika taarifa na ofisi yake ilisema kiongozi huyo wa Ethiopia anaanza tena uongozi wa vita huku nchi hiyo "ikiendelea kupata mafanikio muhimu dhidi ya TPLF", chama tawala cha zamani ambacho kinapambana na serikali.

"Vikosi vya Ethiopia vikiongozwa na Waziri Mkuu, ambaye ameelekea mbele tena, wameshazingira milima ya Zobel, miji ya kimkakati ya Arjo, Fokisa, Boren ... na kufunga barabara kuu ya Woldia-Mekelle," ofisi yake ilisema kupitia mtandao wa Twitter siku ya Jumapili.

Hata hivyo madai haya ya kuwa mstari wa mbele hayataweza kuthibitishwa kutokana na kuzuiliwa kwa waandishi wa habari kufika mstari wa mbele pamoja na kukatwa kwa mawasiliano katika sehemu kubwa ya eneo la vita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live