Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu Congo agoma kupiga picha na Rais Kagame

Congo Rwanda Mgomo Waziri Mkuu Congo agoma kupiga picha na Rais Kagame

Mon, 21 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi wa nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa wamefanya mkutano katika kisiwa cha Djerba nchini Tunisia kujadili ongezeko la ukosefu wa utulivu katika nchi za Afrika zinazozungumza Kifaransa.

Mkuu wa kikundi hicho, Louise Mushikiwabo, alisema kulikuwa na mijadala mirefu kuhusu maeneo makuu ya migogoro.

Alisema kundi hilo linaweza kuunga mkono na kuharakisha juhudi "kupatanisha pande zinazozozana".

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jean-Michel Sama Lukonde, alikataa kupiga picha ya pamoja karibu na rais wa Rwanda, Paul Kagame.

Kinshasa imemshutumu kwa kuunga mkono waasi wa M23 wanaopigana mashariki mwa DR Congo.

Rwanda imekuwa ikikanusha madai hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live