Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu Burundi atua tayari kushuhudiwa JPM akiapishwa

5190fe85ec5579ca08b99c1bdde973c4 Waziri Mkuu Burundi atua tayari kushuhudiwa JPM akiapishwa

Wed, 4 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI Mkuu wa Burundi, Alain Bunyon amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam, mchana wa leo kuja kushiriki shughuli ya kuapishwa kwa awamu ya pili ya Rais John Pombe Magufuli hapo kesho jijini Dodoma.

Kiongozi huyo ni mmoja ya viongozi wa juu kutoka mataifa ya nje wanaokuja kuungana na maelfu ya watanzania kushuhudia tukio hilo litakalofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Serikalini viongozi zaidi wanategemewa kuwasili hapa nchini hii leo kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo.

Tanzania hivi karibuni ilifanya uchaguzi mkuu wa sita tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi ambapo Rais Magufuli alishinda kwa asilimia 84 ya kura zilizopigwa.

Chanzo: habarileo.co.tz