Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Matiang'i ametaja mali za Naibu Rais Ruto zinazolindwa na serikali

Eda36b50ea0ba55c Waziri Matiang'i ametaja mali za Naibu Rais Ruto zinazolindwa na serikali

Wed, 1 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i amefichua baadhi ya mali zinazomilikiwa na Naibu Rais William Ruto ikiwemo makazi yaliyojengwa kwa ekari 22,000, jumba la kuegesha helikopta na makazi mengine ya kibinafsi.

Akiongea mbele ya kamati ya Bunge Jumatano, Septemba 9, Matiang'i alisema maafisa 51 wanalinda mali nyingine 10 za RutoKituo cha gesi cha Kitengela kina maafisa sita, hoteli ya kifahari ya Weston ina maafisa wanne na shamba la Murumbi lina maafisa sita.

Waziri huyo alidokeza kuwa naibu rais wa sasa analindwa zaidi ikilinganishwa na watangulizi wake tangu uhuru

Waziri huyo aliyasema haya mbele ya Kamati ya Bunge kuhusiana na Usalama Jumatano, Septemba 1 ambapo alidokeza kuwa naibu rais wa sasa analindwa zaidi ikilinagnishwa na watangulizi wake tangu uhuru.

Matiang'i alifichua kwamba kwa jumla Ruto ana walinzi 257 na kwa sasa anapewa ulinzi wa VVIP wa kikosi spesheli cha maafisa 74 wa kumlinda rais na maafisa wengine 183 kutoka idara mbali mbali wanaolinda makazi yake.

Matiang’i aliiambia kamati hiyo kwamba maafisa sita wanalinda kituo chake cha gesi mtaani Kitengela, 4 katika shamba la Murumbi lenye ekari 395 huko Transmara Narok na wengine 6 wanaolinda shamba la DP la ekari 6,073- ADC Laikipia Mutara Ranch.

Mali zingine zilizoorodheshwa zinazolindwa na maafisa wa polisi ni: Hoteli ya Dolphine, Mombasa (LR. MN / 1/3266) -3 Ekari (6), Shamba la Mata - Taita Taveta (LR. 10287/10 & 11) Ekari 2,537 (6), Makazi ya Kibinafsi Elgon View Eldoret (4).

Shamba la Kuku la Koitalel Eldoret (4), Makaazi ya Kibinafsi eneo la Kosachei Eldoret (Magereza 3, 1 AP), Kwae Island Development Ltd - Uwanja wa ndege wa Wilson (majumba mawili ya kuegesha helikopta 5) (5)

Hii ni pamoja na maafisa wengine 121 kutoka Polisi wa Utawala (AP) na Huduma za Magereza ambao wanatoa usalama katika makazi mbali mbali ya DP.

Akitoa mwanga mabadiliko ya usalama wa DP, Waziri wa Mambo ya Ndani alisema makaazi ya DP sio sehemu ya kile kinachoonekana kama 'eneo linalolindwa' ambapo maafisa wa GSU hutoa usalama.



"Nyumba ya DP Ruto sio nyumba ya kulala ya wageni wa serikali au Ikulu, sheria iko wazi ni makazi yake …… sisi katika sekta ya usalama tunafanya kazi inavyopaswa kufanywa na wala so kujitafutia umaarufu," CS Matiang'i alielezea.

Wakati uo huo, Matiang'i alifafanua kwamba Rais Uhuru Kenyatta na Naibu Rais William Ruto, wanalindwa na vikosi tofauti chini ya kitengo spesheli cha kumpa ulinzi rais.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke