Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mambo ya Nje Marekani kuzuru Ethiopia

Waziri Nje Marekani.jpeg Waziri Mambo ya Nje Marekani kuzuru Ethiopia

Sun, 12 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken anatarajiwa kuizuru Ethiopia wiki ijayo kujadili utekelezwaji wa makubaliano ya amani yaliositishwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini, wizara hiyo imeeleza.

Haijabainika wazi iwapo atasafiri kuelekea katika eneo la kaskazini lililoathirika na vita Tigray. Huenda ziara hii ikawa ishara nzuri kwa nchi hiyo, iliokabiliwa na vikwazo vya Marekani wakati vita vikidumaza uhusiano kati ya mataifa hayo yaliokuwa washirika wa karibu.

Blinken pia atakutana na mkuu wa Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat mjini Addis Ababa kujadili "malengo makuu ya kieneo na kimataifa," kwa mujibu wa ofisi yake.

Makubaliano ya amani ya Ethiopia yalitiwa saini mnamo Novemba kati ya serikali na wapiganaji wa Tigray kufuatia mzozo wa miaka miwili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live