Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Magoha atangaza kuanza kusahihishwa kwa mtihani wa KCSE

C4092960f275d673 Waziri Magoha atangaza kuanza kusahihishwa kwa mtihani wa KCSE

Sun, 18 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Zoezi la kuusahihisha Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE) litaanza katika muda wa wiki tatu zijazo.

Waziri wa Elimu George Magoha alisema Ijumaa, Aprili 16 kwamba mikakati yote ya usalama imewekwa tayari huku zoezi hilo likitarajiwa kung'oa nanga.

Akizungumza katika kituo cha kuhifadhi katarasi zaa mtihani huko Naivasha, Magoha alisema walimu wote watakaoshiriki zoezi hilo watapimwa dhidi ya virusi vya corona.

"Serikali inakusudia kuwachanja walimu wote, hususan wale ambao wana umri wa zaidi ya miaka 58 lakini tutaanza na wanaoshiriki kuusahihisha mtihani," Magoha alisema.

Prof Magoha alisema kuwa licha ya kukamatwa kwa baadhi ya maafisa wasimamizi kuhusiana na wizi wa mtihani, walimu na maafisa wa usalama walitekeleza jukumu lao ipasavyo.

"Tulikuwa na matukio mabaya ambapo baadhi ya walimu walichapisha mtihani kwenye mitandao ya kijamii, na tumewatambua. Wale ambao walitekeleza kikamilifu majukumu tao kikamlifu wakati mitihani ikiendelea watatuzwa," alisema Magoha.

Wakati uo huo, magoha alisema tayari mikakati inapangwa kuwawezesha wanafunzi waliomaliza mitihani na ambao wanataka kusafiri katika kaunti zilizofungwa kufika makwao.

"Kaunti tano zimefungwa lakini tumepanga na maafisa wa usalama kuwawezesha watahiniwa kusafiri," Waziri huyo alisema.

Matamshi ya Magoha yaliwadia siku moja tu baada ya kutangaza matokeo ya Mtihani wa Kitaiofa wa Shule za Msingi (KCPE).

Alibainisha matokeo ya 2020 yalikuwa bora ikilinganishwa na yale ya 2019.

Watahiniwa milioni 1,179,182 walifanya mtihani wa KCPE kati ya Machi 22 na Machi 24, 2021.

Watahiniwa 590,450 walikuwa wavulana wanaowakilisha asilimia (50.07%) nao wasichana walikuwa 588,742 ambapo ni asilimia (49.93%).

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke