Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazee wapiga kura zao nyumbani Afrika Kusini

Wazee Wapiga Kura Zao Nyumbani Wazee wapiga kura zao nyumbani Afrika Kusini

Wed, 29 May 2024 Chanzo: Bbc

Seipati Julia Ntseie mwenye umri wa miaka 75 alivalia mavazi ya kijani siku mbili zilizopita ili kupiga kura nyumbani.

Anaishi katika kitongoji cha Alexandra huko Johannesburg na kama vitongoji vingine vya miji ambapo watu wengi walilazimishwa kuishi wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi, upigaji kura unaweza kuwa changamoto kwa mtu mzee au mtu mwenye ulemavu.

Hii kwa sababu katika maeneo hayo, vituo vingi vya kupigia kura haviko katika umbali wa kutembea au kufikiwa kwa urahisi kupitia usafiri wa umma.

Kwa hivyo Tume Huru ya Uchaguzi (IEC) huwatuma maafisa kwenye makazi yao wakiwa wamebeba karatasi na masanduku ya kupigia kura. Hii ilitokea Jumatatu.

"Nina furaha kwamba IEC bado inatukumbuka na hututembelea nyumbani," Nteseie aliiambia BBC. Maafisa wa uchaguzi pia walitembelea baadhi ya majirani zake, ambao pia walihitaji usaidizi wa kupiga kura zao. Jumla ya Waafrika Kusini 295,731 walijiandikisha kupiga kura wakiwa nyumbani au maeneo mengine ya makazi, kama vile hospitali, vituo vya wazee au vituo vya huduma za afya kwa sababu ya umri wao au udhaifu.

Chanzo: Bbc