Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazambia waomboleza kifo cha mwimbaji wa nyimbo za injili makanisani na vilabuni

Wazambia Waomboleza Kifo Cha Mwimbaji Wa Nyimbo Za Injili Makanisani Na Vilabuni.png Wazambia waomboleza kifo cha mwimbaji wa nyimbo za injili makanisani na vilabuni

Mon, 5 Aug 2024 Chanzo: Bbc

Baadhi ya wanamuziki wakubwa nchini Zambia wametumbuiza katika tamasha la kuomboleza kifo cha mwimbaji wa nyimbo za Injili Matthew Ngosa mwenye umri wa miaka 46, siku moja kabla ya kuzikwa kwake katika mji mkuu, Lusaka.

Watazamaji walijiunga na kuvitangaza vibao vyake alivyovipenda sana katika kanisa la Praise Christian Centre. Huo ndio ulikuwa umaarufu wa baadhi ya nyimbo zake ambazo hazikupigwa tu makanisani bali pia katika vilabu vya usiku kwa kipindi cha miongo miwili.

Ukumbi wa Lusaka ulikuwa umejaa mashabiki, marafiki, familia na maafisa wa serikali. Kaka yake Boyd, pia mwanamuziki, maarufu kama BJ, aliwaongoza waombolezaji.

Matthew alianza kuimba na BJ na mdogo wake Hezron walipokuwa bado shule ya sekondari, mara nyingi wakiimba cappella.

Walijua walitaka kufanya kazi ya muziki, matarajio ambayo rahisi katika nchi ambayo uharamia hufanya wanamuziki wengi kupata pesa kidogo kutoka kwenye muziki wao. Matthew na Hezron waliitwa The Ezma Brothers ndani ya kundi kubwa linalojulikana kama The Tribe Called Christians. Baadaye, katika Kanisa la Northmead Assemblies of God la Lusaka, Matthew alijiunga na Kwaya ya The Christ Ambassador, ambako aliboresha ujuzi wake. Mnamo 2004 alitoa albamu yake ya kwanza yenye mafanikio makubwa ya Umutima Wandi (Moyo Wangu), ambayo ilitawala chati za muziki. Nyimbo za Injili zikiwemo Ukololela na Ndakunkula zilifuata , hizo mbili pia zikawa nyimbo za kutumbuiza kwenye vilabu. Matthew Ngosa hakuwahi kutajirika, lakini aliweza kujikimu kimaisha kutokana na vibao vyake kabla ya kugundulika kuwa na saratani ya ini mwezi Januari.

Chanzo: Bbc