Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili mbaroni kwa tuhuma za kuiba kichanga

Kichanga Pic Wawili mbaroni kwa tuhuma za kuiba kichanga

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi katika mji wa Masaka wanawashikilia wanawake wawili kwa kudaiwa kumuiba mtoto mchanga katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Masaka.

Charity Mbabazi ambaye ni mama wa mtoto alipozungumza na Daily Monitor amesema kabla ya kumuiba, wanawake hao wawili ambao hakuwa anawafahamu walimkaribisha alipofika katika wodi ya wazazi, Januari 12, 2024.

Baada ya kukaribishwa, alipojifungua alikaribishwa kwa tabasamu na mama mwingine aliyetambuliwa kwa jina la Aisha Naluyange (mmoja wa watuhumiwa), ambaye alimweleza kuwa yeye pia alijifungua mtoto lakini mwanaye alipelekwa chumba cha uangalizi maalumu, baada ya kupata tatizo la kupumua.

New Content Item (6)

"Nilipomuuliza jinsi anavyomnyonyesha mtoto wake, Naluyange alisema wauguzi humwita kumnyonyesha wakati mtoto anapotaka kunyonya," amesema Charity.

Charity ameendelea kusema kuwa wakati mumewe alipokwenda kumtembelea hospitalini hapo, alishauriwa kutafuta nguo mpya kwa ajili ya mtoto na hapo ndipo Naluyange alitumia fursa hiyo kwa kuwashauri wote wawili kwenda pamoja kuchagua nguo nzuri na atawaangalizia mtoto wao. "Tuliporudi wodini, mtoto wetu alikuwa hayupo. Lakini Naluyange alikuwepo na alituambia kuwa mtoto amepelekwa kwenye mashine maalumu baada ya kupata matatizo. “Tulipoenda kwenye chumba kile hatukumuona mtoto wetu. Hapo ndipo tuliomba msako wa mtoto aliyeibiwa kufanyika," Charity amesimulia.

Amesema, Naluyange alishirikiana na Zainab Assimwe (mtuhumiwa mwingine) kuchukua mtoto na kujaribu kutoka naye nje ya hospitali.

Bahati nzuri, Asiimwe alizuiliwa na walinzi katika geti la kutokea hospitalini hapo kwa kukosa fomu ya ruhusa, jambo ambalo lilifanya wakamatwe.

Ofisa mkuu wa uchunguzi wa jinai katika kituo cha kati Masaka, Richard Tusingwire amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, huku akieleza kuwa tayari Asiimwe na Naluyange wanashikiliwa ili kusaidia uchunguzi.

"Wako nasi wakati huu uchunguzi ukiendelea. Na tutakapomaliza, tutawapeleka mahakamani kujibu mashtaka ya wizi na biashara ya watoto," amesema Ofisa huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live