Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili mahakamani Kenya kwa kumuua mwanariadha wa Uganda

Wawili Mahakamani Kenya Kwa Kumuua Mwanariadha Wa Uganda Wawili mahakamani Kenya kwa kumuua mwanariadha wa Uganda

Tue, 2 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Washukiwa wawili wamefikishwa mbele ya mahakama mjini Eldoret kuhusu mauaji ya mwanariadha Edward Kiplangat almaarufu Benjamin.

Washukiwa hao wawili ni pamoja na David Ekhai Lokere almaarufu Timo mwenye umri wa miaka 25 na Peter Ushuru Khalumi mwenye umri wa miaka 30.

Walifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu Kesse Cherono ambaye aliwaruhusu polisi kuwazuia washukiwa hao kwa siku 21 ili kuwezesha upelelezi kukamilika.

Cherono alisema alikuwa amezingatia ukweli kwamba amani ya umma ilivurugwa kufuatia tukio hilo. Afisa Mkurugenzi wa mashtaka Inyasio Mwaniki anayeishi katika kaunti ndogo ya Moiben huko Uasin Gishu alikuwa ameiambia mahakama kuwa bado wanachunguza kisa hicho.

Alisema mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa kwenye dimbwi la damu ukiwa na majeraha ya mapanga. Alisema wawili hao walikamatwa mnamo Januari 1, 2024, Eldoret na Kitale na wanashukiwa kumuua mwanariadha huyo.

"Bado hatujafanya uchunguzi wa marehemu na vielelezo muhimu vilivyokusanywa kutoka kwa washukiwa bado havijachukuliwa ili kuchunguzwa na wakemia wa serikali," afisa huyo wa DCI alisema.

Alisema picha za CCTV kutoka eneo la uhalifu pia bado hazijachambuliwa na kitengo cha uhalifu wa mtandao.

Afisa huyo wa DCI pia alibaini kuwa rekodi za simu za mkononi pia hazijachukuliwa pamoja na nambari za usajili za gari na pikipiki iliyopatikana katika eneo la tukio.

Mwaniki alisema pia bado hawajaandika taarifa kutoka kwa mashahidi katika eneo la tukio. Aliongeza kuwa taarifa muhimu kutoka kwa ubalozi wa Uganda kuhusu hali ya marehemu kabla ya kifo chake bado hazijafahamika.

“Ni kwa ajili ya haki walalamikiwa kuzuiliwa kwa siku 21 ili kuwezesha upelelezi kukamilika,” alisema ofisa huyo.

Wakili George Sonkule wa mshtakiwa alinukuu Muswada wa Haki katika Katiba akisema kuwa washukiwa wana haki ya uhuru.

Chanzo: Bbc