Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wavunja duka na kuiba whiskey baada ya pombe kupigwa marufuku Afrika Kusini

Ombe Pombe

Wed, 15 Jul 2020 Chanzo: BBC

Siku mbili baada ya Afrika Kusini kurejesha marufuku ya kununua pombe kupambana na kusambaa kwa virusi vya corona, wezi walivunja kwenye duka moja la vilevi mjini Cape town.

''Kimsingi wamechukua Whisky zote , Mark Kallend, mmiliki wa duka la vinywaji vya kilevi Liquor Bothasig, aliambia News 24 kuhusu tukio hilo mapema asubuhi siku ya Jumanne.

''Waling'oa lango la kuingilia kwa kutumia gari lao…wakafunga kamba kulizunguka kisha wakaling'oa. Kisha walirusha jiwe zito dirishani,'' alisema.

''Chupa za mvinyo na brandy hazikuguswa'', aliongeza.

Bwana Kallend amesema tukio hilo limeonesha jinsi watu walivyo katika hali ya kukata tama.

Katika hotuba yake siku ya Jumapili Rais Cyril Ramaphosa alisema kupigwa marufuku kwa pombe - hatua ya pili mwaka huu kutapunguza mzigo kwa mfumo wa afya nchini humo.

Zaidi ya 40% ya watu 40,000 wenye matatizo ya kiakili yaliyorekodiwa nchini humo katika kipindi cha juma moja yanahusiana na matumizi ya vilevi, jambo ambalo mfumo wa afya hauwezi kugharamia kwa sasa.

Linapokuja suala la virusi vya corona, Afrika Kusini ni nchi iliyoathirika zaidi barani Afrika ikiwa na wagonjwa zaidi ya 275,000.

Vifo vilivyotokana na Covid-19 pia vimeongezeka na kuwa zaidi ya 4,000 na serikali inakisia kuwa idadi inaweza kufikia 50,000 mwishoni mwa mwaka.

Chanzo: BBC