Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waumini wadai kunyanyaswa kingono kanisa la TB Joshua

TB Joshua?fit=650%2C350&ssl=1 Waumini wadai kunyanyaswa kingono kanisa la TB Joshua

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa imefichua unyanyasaji na mateso yanayodaiwa kufanywa na mwanzilishi wa mojawapo ya makanisa makubwa zaidi duniani, marehemu TB Joshua.

Taarifa hiyo iliyotolewa jana na shirika la habari la BBC imeeleza kuwa makumi ya waumini wa zamani wa Kanisa la Synagogue Church of all Nations (SCOAN) wakiwemo Waingereza watano, wamedai kwa zaidi ya miaka 20, marehemu TB Joshua aliwafanyia ukatili, ikiwa ni pamoja na ubakaji na kutoa mimba kwa lazima, katika makazi yake ya siri jijini Lagos.

TB Joshua alifariki dunia Juni, 2021. Alisifiwa kama mmoja wa wachungaji wenye ushawishi mkubwa katika historia ya Afrika, akiongoza watu mashuhuri, wakiwemo wanasiasa wakubwa.

TB Joshua, mmoja wa viongozi wa dini aliyekuwa na ushawishi mkubwa barani Afrika na mmoja wa wachungaji tajiri zaidi ni mwanzilishi wa kanisa hilo kubwa la ghorofa 12 lililoko Ikotun, Jimbo la Lagos, ambako aliishi pamoja na wafuasi wake wengi.

Alikuwa maarufu kwa miujiza ambayo ilimzolea idadi kubwa ya wafuasi kote ulimwenguni, ikiwemo uponyaji wa maradhi kama vile Ukimwi, saratani na upofu wa kudumu.

Miujiza hiyo na utabiri wake ulivuta hisia za wengi na kuanza kupata umaarufu mkubwa mwishoni mwa miaka ya 1990 na mwanzoni mwa 2000.

Wafuasi wake wengi walivutwa na ufadhili wake, lakini wengi wao walimfuata kwa kile kilichotajwa kuwa ni miujiza yake.

Hata hivyo, Kanisa la Scoan halikujibu madai hayo, lakini lilisema madai hayo ya awali hayana uhalisia.

Uchunguzi wa miaka miwili wa BBC, kwa ushirikiano na jukwaa la kimataifa la vyombo vya habari, Open Democracy, uliwahusisha zaidi ya wanahabari 15 wa BBC katika mabara matatu.

Uchunguzi wa BBC ulihusu madai ya unyanyasaji wa kijinsia, unyanyasaji wa kimwili, kufungwa na miujiza ya uwongo.

Wanawake wengi walidai walinajisiwa na walibakwa mara kwa mara kwa miaka mingi katika makazi waliyokuwa wakiishi na Joshua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live