Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waumini wa Rastafari wataka waruhusiwe kutumia bangi kufanya ibada

67ebd0e9fcb98d00 Waumini wa Rastafari wataka waruhusiwe kutumia bangi kufanya ibada

Tue, 18 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Waumini wa dini ya Rastafari (RSK) siku ya Jumatatu, Mei 17, waliwasilisha kesi kortini wakitaka matumizi ya bangi ihalalalishwe

- Waumini wa Urastafari walihoji kuwa bangi ni dawa yenye nguvu za kiroho zinazowawezesha kuwasiliana na Mungu moja kwa moja

- Waumini hao pia walizua kwamba haki zao kikatiba za uhuru wa kuabudu zinakandamizwa kinyume na Katiba ya 2010

Waumini wa dini ya Rastafari (RSK) siku ya Jumatatu, Mei 17, waliwasilisha kesi kortini wakitaka matumizi ya bangi ihalalalishwe wakidai kuwa inawasaidia wanapoabudu.

Waumini hao, kupitia wakili wao Shadrack Wamboi, walihoji kuwa bangi ni dawa yenye nguvu za kiroho zinazowawezesha kuwasiliana na Mungu moja kwa moja.

Kwa mujibu wa Taifa Leo, walilalamika kuwa sheria ya kupambana na ulanguzi wa dawa za kulevya iliyopitishwa mwaka wa 1994 inawabagua.

Waumini hao pia walizua kwamba haki zao kikatiba za uhuru wa kuabudu zinakandamizwa kinyume na Katiba ya 2010.

Kiongozi wa imani hiyo Nabii Mwendwa Wambua (Ras Prophet) wanataka mahakama iwasilishe kesi yao kwa kaimu Jaji Mkuu Philomena Mwilu ili abuni jopo la majaji watatu ambalo litasikiliza kesi hiyo.

Kesi hiyo itatengewa siku ya kusikilizwa na Jaji katika idara ya kuamua kesi za haki za binadamu.

Kuhalalishwa kwa BangiMnamo Disemba 2020, Umoja wa Mataifa uliondoa bangi katika orodha ya dawa hatari za kulevya.

Tume ya Umoja wa Mataifa inayosimamia masuala ya mihadarati iliidhinisha pendekezo la Shirika la Afya Duniani (WHO) la kuondoa mmea huo katika kundi la dawa za kulevya linalojumuisha mihadarati mingine kama vile heroin.

Hata hivyo, bangi bado ingali katika orodha ya dawa za kulevya na japo imeshushwa daraja, na mataifa yangali huru kujiamulia kuhusu jinsi ya kudhibiti matumizi yake.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke