Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wauguzi 16 wapoteza maisha kwa covid-19

05a4b4dd90e7e6d78c3112413ebe44c1 Wauguzi 16 wapoteza maisha kwa covid-19

Tue, 22 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WIZARA ya Afya imesema wauguzi 16 wamepoteza maisha, wakiwa ni miongoni mwa wauguzi 945 walioambukizwa ugonjwa wa covid-19 tangu kutangazwa kuingia janga hilo nchini Kenya Machi, mwaka huu.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, katika kipindi cha kati ya Machi hadi sasa, wauguzi 945 wameambukizwa ugonjwa wa covid-19 na 16 kati yao wamepoteza maisha.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Mercy Mwangangi, ameeleza kwamba, wanapokuwa kwenye mstari wa mbele kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona, wauguzi pia wanakabiliwa na hatari ya kuambukizwa magonjwa kama vile homa ya manjano, kifua kikuu na virusi vya Ukimwi.

Kwenye ujumbe wake wa maadhimisho ya siku ya kutambua usalama wa wagonjwa ulimwenguni mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus, alisisitiza umuhimu wa kuzingatia usalama wa wauguzi ili kuwaweka wagonjwa salama

. “Mmoja kati ya wagonjwa 10 wanaolazwa hospitalini hupita huduma isiyo salama. Hili ni tatizo kwa mataifa yote, mataifa tajiri na yale masikini.

Njia mojawapo ya kuwaweka wagonjwa salama ni kwa kuwaweka wauguzi salama. Janga la covid-19 limetukumbusha sisi sote kuhusu jukumu muhimu wanalotekeleza wauguzi katika kutibu na kuyaokoa maisha,” alisema Ghebreyesus.

Ingawa serikali ya Kenya imekuwa ikisema inachukua hatua kuhakikisha wauguzi wanalindwa wakati huu wa janga na covid-19, wauguzi wanaishinikiza kuwalipa mishaara na marupurupu yao, baadhi wakidai tangu Julai, mwaka huu.

“Kwa nini tunateseka kiasi hiki kama wafanyakazi na kama Wakenya? Hatupokei huduma tunazohitaji ilhali kuna uongozi katika nchi hii,” alisema Dk Mwachonda Chibanzi, ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu wa Muungano wa Madaktari Kenya

Chanzo: habarileo.co.tz