Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu zaidi ya laki mbili wamepoteza maisha kwa COVID-19 barani Afrika - AFP

AFP REPORT Vifo zaidi ya 200,000 vya ripotiwa tangu kutoke kwa COVID-19 barani Afrika

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Uchunguzi ya AFP, umeripoti taarifa ya vifo barani Afrika vilivyotokana na janga la UVIKO-19 tangu ulipotangazwa kuingia barani humu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa zaidi ya vifo 200,000 vimetokea tangu kuzuka kwa ugonjwa huu unaotikisa dunia yote kwa sasa.

Utafiti huo umeeleza kuwa nchi 54 za barani humu zinakadiriwa kutoathirika zaidi na virusi hivyo, katika bara lenye watu zaidi ya bilioni 1.3, idadi hiyo ya vifo inatajwa kuonesha ahueni tofauti n amakadirio ya awali yaliyo kisiwa na Mataifa ya Magharibi kuhusu athari za mlipuko wa ugonjwa barani humu.

Hata hivyo Utafiti huo umesisitiza kwa uwazi kuhusu umuhimu wa chanjo ya UVIKO-19, kwa kuwashi viongozi wa serikali zote barani hyumu kuhakikisha wanawasihi wananchi kupata chanjo hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live