Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu wenye silaha wawateka Wakorea, kuua wanajeshi wa Nigeria

Watu Wenye Silaha Wawateka Wakorea, Kuua Wanajeshi Wa Nigeria Watu wenye silaha wawateka Wakorea, kuua wanajeshi wa Nigeria

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Watu wenye silaha wasiojulikana walivizia msafara wa kampuni ya kutoa huduma ya mafuta katika jimbo la Rivers kusini mwa Nigeria na kuwateka nyara wafanyakazi wawili wa Korea Kusini na kuwaua wanajeshi wanne.

Msafara huo ulishambuliwa Jumanne kando ya barabara karibu na Ahoada/Abua, Mashariki-Magharibi katika jimbo hilo.

Wakorea hao walikuwa miongoni mwa wafanyakazi wa Daewoo Engineering and Company - kampuni ya Korea Kusini - ambao walikuwa wakisindikizwa kazini na wanajeshi wa Nigeria.

Madereva wawili pia waliripotiwa kuuawa katika shambulio hilo.

Jeshi la Nigeria limethibitisha kuuawa kwa wanajeshi hao na kutekwa nyara kwa raia hao kutoka nje ya nchi.

Katika taarifa yake, Meja Jonah Danjuma, msemaji wa jeshi, alisema wanajeshi wanawasaka washambuliaji hao ili kuwapata wafanyakazi hao wawili waliotekwa nyara.

Jeshi lililaumu watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo kwa kutekelezashambulio hilo lakini hakuna madai ya kuhusika kwao yaliyotolewa.

Utekaji nyara wa kutafuta kulipwa fidia hutokea mara kwa mara kote nchini Nigeria.

Chanzo: Bbc