Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu wengine 991 wamepatikana na COVID-19, 26 wapoteza maisha

899562d43df31a4a Watu wengine 991 wamepatikana na COVID-19, 26 wapoteza maisha

Tue, 13 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wizara ya afya imetangaza kwamba watu wengine 991 wamepatikana na virusi vya COVID-19 baada ya sampo 6, 417 kufanyiwa vipimo chini ya saa 24 zilizopita

Kufikia sasa, jumla ya visa vya maambukizi vilivyoripotiwa nchini ni 147,147, ilhali sampo zilizopimwa kwa jumla ni 1,571,244.

Kati ya visa vilivyoripotiwa hii leo, 956 ni Wakenya ilhali 35 ni raia wa kigeni, 543 ni wanaume na 448 ni wanawake. Mgonjwa mdogo ana umri wa miezi saba na mkubwa ana miaka 99.

Hata hivyo, wagonjwa wengine 26 wamepoteza maisha yao kutokana na virusi hivyo kwa muda wa 24 zilizopita na kufanya idadi ya vifo kwa jumla kufikia 2, 394.

Wagonjwa wengine 370 wamepona kutokana na virusi hivyo, 214 walikuwa chini ya uangalizi wa kimatibabu wa nyumbani ilhali 156 wameruhusiwa kuondoka katika hospitali mbali mbali.

Kulingana na takwimu za wizara ya Afya, jumla ya wagonjwa waliopona nchini ni 99, 580.

Kwa sasa jumla ya wagonjwa 1,607 wamelazwa katika hospitali mbali mbali kote nchini, 5, 996 wanapokea matibabu wakiwa wamejitenga manyumbani, 239 wamo kwenye ICU na 47 wamewekwa kwenye ventileta.

Kwa mujibu wa wizara ya afya, watu 526, 026 walikuwa wamepokea chanjo ya Astrazeneca kufikia siku ya Jumatatu, Aprili 12, 2021.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke