Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu wengine 287 wapatikana na virusi vya COVID-19 huku 152 wakipona

102628 Pic+kenya+corona Watu wengine 287 wapatikana na virusi vya COVID-19 huku 152 wakipona

Tue, 29 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Watu wengine 287 wamepatikana na virusi vya COVID-19 baada ya sampo 2, 699 kufanyiwa vipimo chini ya saa 24 zilizopita, kwa sasa asilimia ya maambukizi imefikia 10.6%.

Kati ya visa vilivyoripotiwa, 280 ni Wakenya ilhali saba ni rais wa nchi za kigeni, kijinsia 170 ni wanaume na 117 ni wanawake.

Mgonjwa mdogo ana umri w miezi mitatu ilhali mkubwa ana miaka 89.

Kufikia sasa visa vya maambukizi vilivyoripotiwa nchini vimefikia 182,884 na sampo zilizopimwa kwa jumla ni 1,945,736.

Wagonjwa 152 wamepona kutokana na virusi hivyo , kati yao 84 walikuwa wakipokea matibabu wakiwa chini ya utunzi wa kimatibabu nyumbani ilhali 68 walikuwa wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini.

Kwa jumla wagonjwa waliopona nchini ni 124,588 kulingana na takwimu za Wizara ya Afya.

Watu wengine 17 wamepoteza maisha yao kutokana na virusi hivyo chini ya saa 24 zilizopita na kupelekea idadi ya vifo nchini kufikia 3,612.

Wagonjwa wengine 1,062 wamelazwa katika hospitali mbali mbali.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke