Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu watatu wauawa katika hujuma ya kigaidi Mogadishu, Somalia

Mogadishu, Somalia Watu watatu wauawa katika hujuma ya kigaidi Mogadishu, Somalia

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlipuko mkubwa umetikisa wilaya ya Hamarweyne ya Mogadishu na kuua watu watatu.

Kulingana na mamlaka za eneo hilo, mshambuliaji alijilipua alipokuwa akifuatwa na maafisa wa usalama waliokuwa wanashuku ni gaidi.

Wasimamizi wa usalama wamethibitisha kuwa mlipuko huo umesababisha vifo vya watu watatu na kuwaacha wengine wawili wakiwa wamejeruhiwa. Maafisa wa usalama walifika haraka eneo la tukio kuanzisha uchunguzi kuhusu hujuma hiyo ya kigaidi.

Kundi la wanamgambo la al-Shabaab limedai haraka kuhusika na shambulio hilo. Kundi hilo limedai katika taarifa yake kuwa lengo lao ni watu binafsi wanaofanya kazi serikalini, na kusema kuwa mlipuko huo ulifanywa na mwanachama wa kundi hilo ambaye alijiua kwa kukusudia.

Somalia imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa usalama kwa miaka mingi, huku vitisho vikuu vikitoka kwa al-Shabaab na makundi ya kigaidi ya Daesh/ISIS.

Al-Shabaab wamezidisha mashambulizi tangu rais wa Somalia, ambaye alichaguliwa kwa muhula wa pili mwaka jana, kutangaza "vita vya hali ya juu" dhidi ya kundi hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live