Mwanaume mwenye umri wa miaka 60 alikuwa amefungwa kwa kamba na koo lake lilikatwa, nyumba yake ilichomwa pamoja na vitu vyote. Watu wengine watatu waliuawa kwa namna sawa na hiyo huku mwathiriwa wa tano akipigwa risasi
Washambuliaji pia walichoma nyumba na kuharibu mali. Polisi walielezea tukio hilo kama shambulio la kigaidi, maneno ambayo kwa kawaida hutumiwa kutaja uvamizi wa kundi la al-Shabab lenye makao yake Somalia.
Lamu iko karibu na mpaka wa Kenya na Somalia na wapiganaji kutoka kundi la al-Shabab mara kwa mara hufanya mashambulizi katika eneo hilo, kama sehemu ya juhudi za kuishinikiza Kenya kuondoa wanajeshi wake kutoka Somalia, mahala ambako ni sehemu ya kikosi cha kimataifa cha kulinda amani kinachoilinda serikali kuu.
Polisi wanasema kundi la washambuliaji lilishambulia vijiji vya Salama na Juhudi mapema Jumapili asubuhi.
Mwanaume mwenye umri wa miaka 60 alikuwa amefungwa kwa kamba na koo lake lilikatwa, nyumba yake ilichomwa pamoja na vitu vyote. Watu wengine watatu waliuawa kwa namna sawa na hiyo huku mwathiriwa wa tano akipigwa risasi.
Nyumba za watu waliouawa na wakaazi wengine zilichomwa moto katika shambulio hilo na washambuliaji hao walitoweka katika msitu ulio karibu, polisi wamesema.
Kundi la al-Shabab lenye uhusiano na al-Qaida limekuwa likipigana kwa miaka kadhaa nchini Somalia kuiangusha serikali kuu na kuanzisha utawala wake kwa kuzingatia tafsiri yake kali ya sharia ya Kiislamu.