Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu watano wafariki baada 'kushikwa mateka' kanisani

KUSINI Watu watano wafariki baada 'kushikwa mateka' kanisani

Sat, 11 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu watano wameuawa baada ya washambuliaji kuvamia kanisa moja Afrika Kusini wakati malumbano yanaendelea juu ya uongozi wa kanisa hilo.

Polisi Afrika Kusini imesema kwamba wamenusuru wanaume, wanawake na watoto waliokuwa wametekwa nyara viungani mwa mji wa Johannesburg Jumamosi asubuhi.

Pia polisi wamewakamata watu karibia 40 na kunasa silaha kadhaa.

Walioshuhudia kisa hicho wanasema kwamba wanaume waliovamia kanisa la International Pentecostal Holiness walikuwa sehemu ya kundi pinzani.

Inasemekana kwamba uongozi wa kanisa hilo ni suala ambalo limekuwa likizua vurugu tangu aliyekuwa kiongozi wa kanisa hilo alipoaga dunia 2016.

2018, polisi waliwahi kuitwa kwenye kanisa hilo kufuatia mashambulio ya risasi miongoni mwa waumini, kulingana na ripoti ya shirika la ILO, Afrika Kusini.

Mwaka jana, fedha za kanisa hilo zilikuwa angalizo baada ya kutokea kwa madai kuwa takriban randi milioni 110 sawa na ($6.5m; £5.2m) hazijulikani zilipo, kulingana nagazeti la The Sowetan .

Jumamosi, polisi waliitwa katika kanisa hilo eneo la Zuurbekom karibu saa tisa mchana saa za eneo.

Kulingana na msemaji wa kikosi cha polisi cha taifa, Brigedia Vish Naidoo, kundi la lililoshambulia lilifahamisha kundi lililokuwa ndani ya kanisa kwamba wanakuja kutwaa udhibiti wa jengo la kanisa

Alisema watu wanne wamepigwa risasi na kuchomwa moto hadi kufa wakiwa ndani ya gari, huku mlinzi wa jengo hilo ambaye inasemekana alijibu shambulio, pia naye amekufa baada ya kupigwa risasi.

Bunduki tano za rashasha, bunduki 16 na bastola 13 pamoja na silaha zingine zimepatikana ndani ya kanisa na kuchukuliwa na maafisa wa polisi kama ushahidi.

Idara ya Polisi ya Afrika Kusini imesema miongoni mwa waliokamatwa ni maafisa wa polisi wa idara hiyo, maafisa wa kikosi cha jeshi la Ulinzi, maafisa polisi wa mji wa Johannesburg pamoja na maafisa wa idara ya huduma ya magereza.

Kanisa la International Pentecostal Holiness linasemekana kuwa na waumini karibu milioni tatu Kusini mwa Afrika .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live