Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu wanaoshukiwa kuwa magaidi waua wanajeshi 12 wa Niger

Watawala Wa Kijeshi Wa Niger Wakutana Na Wajumbe Wa Nigeria Watu wanaoshukiwa kuwa magaidi waua wanajeshi 12 wa Niger

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban wanajeshi 12 wa Niger wameuawa katika shambulizi la kuvizia na watu wanaoshukiwa kuwa magaidi katika kijiji kimoja kusini magharibi mwa Niger, likiwa ni shambulio la hivi punde zaidi tangu Rais Mohamed Bazoum aondolewe madarakani katika mapinduzi ya kijeshi.

Magaidi hao walitekeleza shambulizi hilo la kuvutia dhidi askari wa kikosi cha gadi la walinzi wa taifa Jumapili jioni katika kijiji cha Anzourou katika eneo la Tillaberi.

Gavana wa kijeshi wa jimbo hilo luteni Kanali Maina Boucar, ameiambia televisheni ya taifa kwamba askari wa gadi hiyo wametoa pigo kubwa kwa washambuliaji lakini kwa bahati mbaya, askari 12 wameopteza maisha.

Shambulizi hilo limekuja siku chache baada ya wanajeshi wengine 17 kuuawa wakati watu wenye silaha walipovizia kikosi cha jeshi karibu na mji wa Koutougou katika eneo la Tillaberi karibu na mpaka na Burkina Faso. Jenerali Abdourahamane Tchiani

Wanajeshi, wakiongozwa na Jenerali Abdourahamane Tchiani, kamanda wa zamani wa walinzi wa rais wa Niger, walimuondoa Bazoum madarakni mnamo Julai 26, wakisema kuwa utawala huo ulikuwa umehatarisha usalama wa nchi.

Eneo la Tillaberi linakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya makundi yenye silaha yenye mafungamano na makundi ya kigaidi ya al-Qaeda na Daesh.

Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) wiki iliyopita ililitaka jeshi kurejesha utulivu wa kikatiba nchini Niger "ili kujikita zaidi katika usalama wa nchi hiyo."

Siku ya Jumanne, Umoja wa Afrika ulisema umesimamisha uanachama wa Niger katika jumuiya hiyo hadi jeshi litakapoachia madaraka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live