Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu wanakula mchanga uliochanganywa na ukwaju

Ukwaju Watu wanakula mchanga uliochanganywa na ukwaju

Fri, 4 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Raia wa kusini mwa Madagascar wanakula mchanga uliochanganywa na ukwaju kwasababu ya kiangazi ambacho kimeharibu zao linalotegemewa na wenyeji, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

“Tunauita udongo wenye kuhimili kiangazi kwasababu unaruhusu ukwaju kukua na kutusaidia kukabiliana na kiangazi, siku hizi hatutafuti tena chakula bali tunatafuta mbinu za kupata kitu chochote cha kushikilia tumbo” AFP imemnukuu mkulima wa eneo Doday Fandilava Noelisona.

Matunda ya dungusi ambayo watu huyategemea yamekauka kwasababu ya ukosefu wa mvua.

Aidha, shirika la AFP limemnukuu mkulima mwingine, Avianay Idamy, ambaye anasema amegeukia uuzaji wa makaa kupata pesa za kukidhi mahitaji ya familia yake angalau waweze kula muhogo mara moja tu kwa siku.

Shirika la chakula dunia- WFP, linasema watu milioni 1.5 kusini mwa Madagascar wanahitaji msaada wa dharura wa chakula.

HII NDIO HOTELI YA NYOTA TANO WANAYOLALA WANAFUNZI WA UHASIBU ARUSHA

Chanzo: millardayo.com