Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu sita wauawa shambulio la kujitoa muhanga Somalia

Vikosi Vya Somalia Vinachukua Maeneo Yaliyoachwa Na Wanajeshi Wa AU Watu sita wauawa shambulio la kujitoa muhanga Somalia

Sun, 22 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu sita, wakiwemo raia wawili, wameuawa na wengine tisa kujeruhiwa Jumamosi hii, Oktoba 21, katika shambulio la kujitoa mhanga kwenye kituo cha juu cha kijeshi katika viunga vya mji mkuu wa Somalia Mogadishu, polisi imetangaza.

Shambulio hilo limedaiwa na wanamgambo wa Kiislamu wenye itikadi kali wa Al Shabab. Kwa mujibu wa mashahidi, mshambuliaji wa kujitoa mhanga ameliendesha gari lake lililokuwa na vilipuzi hadi kwenye kituo cha kijeshi cha Ceelasha-Biyaha, katika viunga vya magharibi mwa Mogadishu, na kusababisha mlipuko mkubwa uliosababisha uharibifu mkubwa, ikiwa ni pamoja na nyumba jirani.

"Wakhariji (neno linalotumiwa na mamlaka kutaja Al Shaba), kama wanavyofanya mara kwa mara, walijaribu kuleta gari lililokuwa na vilipuzi na (vipande vya) chuma katika mji wa Mogadishu. Lakini baada ya kunyimwa kibali cha kuingia, walilipua gari hilo katika kambi ya vikosi vya usalama huko Ceelasha-Biyaha,” msemaji wa polisi wa Somalia Sadik Dudishe amesema katika taarifa.

"Miongoni mwa waathiriwa waliorekodiwa, kuna sita waliofariki, askari wanne wa vikosi vya usalama na raia wawili, na majeruhi tisa, wakiwemo raia wanne," ameongeza. Mohamed Sharif, ambaye ni mmoja wa mùashahidi amesema aliona miili ya raia watano. “Nilikuwa ndani ya basi dogo karibu kabisa na eneo la mlipuko, tulikuwa na bahati sana kwamba hakuna abiria hata mmoja kwenye basi hilo aliyejeruhiwa. Niliona miili ya raia watano akiwemo mzee mmoja,” amesema.

Vita kamili

Kundi la Al Shabab lenye mafungamano na Al-Qaeda, limekuwa likiongoza mashambulizi tangu mwaka 2007 dhidi ya serikali ya Somalia, inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa, ili kuanzisha sheria za Kiislamu katika nchi hii ya Pembe ya Afrika.

Wakifukuzwa kutoka katika miji mikuu mwaka 2011-2012, wamesalia imara katika maeneo makubwa ya vijijini katikati mwa nchi na kusini mwa nchi, ambapo mara kwa mara hufanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama, wanasiasa na raia.

Rais Hassan Cheikh Mohamoud ambaye alichaguliwa mwezi Mei 2022, alitangaza "vita kamili" dhidi ya Al Shabab. Vikosi vya serikali na wanamgambo wa koo, wakiungwa mkono na kikosi cha Umoja wa Afrika na mashambulizi ya anga ya Marekani, wamekuwa wakiongoza mashambulizi ya kijeshi katikati mwa nchi hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja, ambayo yamesababisha kutwaa tena maeneo kadhaa. Licha ya vikwazo hivyo, Al Shabab inaendelea kufanya mashambulizi mabaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live