Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu saba wapoteza maisha katika kijiji cha Bana Congo

Watu Saba Wapoteza Maisha Katika Kijiji Cha Bana Congo.png Watu saba wapoteza maisha katika kijiji cha Bana Congo

Wed, 14 Aug 2024 Chanzo: Bbc

Watu saba wamepoteza maisha katika Kijiji cha Bana Congo karibu na Kijiji cha Mungamba jimboni Ituri mashariki mwa DRC, majira ya saa tano usiku.

Taarifa zinaeleza kuwa kikundi cha waasi wa ADF waliingia katika kijiji hicho na kuchoma moto nyumba nane na kusababisha watu kufariki huku wengine wakiwaua kwa kuwakata mapanga.

Mashuhuda wanaeleza kujwa kulikuwepo na dalili za watu hao kuvamia kijiji hicho cha Bana Congo na kuvijulisha vyombo vya usalama lakini hawakuweza kuwasaidia wananchi hao.

Akizungumza na vvyombo vya habari Mtetezi wa haki za binadamu wa eneo hilo Trésor Vweruka amesema hali hiyo inapaswa ikomeshwe kwani watu wasio na hatia wapepoteza maisha.

Hivi karibuni waasi wa ADF wamedaiwa kuua watu zaidi ya 30 katika kijijini Mali ya jame, mpakani mwa Jimbo la Nord-Kivu na ituri.

Chanzo: Bbc