Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu saba wa familia moja wateketea kwa moto

Zimamoto Pic Data Watu saba wa familia moja wateketea kwa moto

Sun, 2 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu saba wa familia moja wameaga dunia kufuatia kisa cha moto kilichotokea usiku wa kuamkia Jumamosi, Oktoba 1, katika kijiji cha Ngimari kaunti ya Embu.

Saba hao ni mwanamume mmoja, mkewe, binti zake wawili, mvulana mmoja na wajukuu wake wawili na waliangamia baada ya moto kuteketeza nyumba yao.

Kwa mujibu wa ripoti, saba hao walichomeka kwa kiasi cha miili yao kutotambulika huku nyumba yao inayoripotiwa kutengenezwa kwa mbao kuteketea kabisa.

Maafisa wa polisi kutoka Runyenjes wamefika eneo la tukio ambalo tayari limejaa wakaazi wa eneo hilo huku hali ya majonzi ikitawala kijiji hicho.

Chanzo cha moto huo bado hakijabainika. Kisa hicho kinajiri wiki moja baada ya nyumba nyingine kuteketea hadi kuwa majivu katika kijiji cha Gikuuri eneo bunge la Runyenjes.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live