Umati mkubwa wa watu umejitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa watu saba wa familia moja ambao walipoteza maisha yao kwa pamoja na watazikwa katika eneo moja huko Ngimari, Embu Mashariki nchini Kenya.
Saba hao ambao ni baba, mke wake, watoto wao watatu na wajukuu wawili walifariki hivi karibuni baada ya nyumba yao iliyotengenezwa kwa mbao kuteketea kwa moto huku miili yao ikishindwa kutambulika vizuri.
Umati mkubwa wa watu waombolezaji na viongozi ulijitokeza jana katika shughuli hiyo kuwapa heshima zao saba hao ambao walipoteza maisha yao kwa uchungu wa kupitiliza.
Gavana wa Embu Cecily Mbarire, naibu wake Kinyua Mugo, mbunge wa Runyenjes Eric Muchangi, Seneta wa Embu Alexander Mundigi na viongozi wengi wanahudhuria mazishi hayo.