Watu wanane wakiwemo saba kutoka familia moja walifariki mjini Cairo Jumatatu wakati jengo la makazi katika mji mkuu wa Misri lilipoporomoka, ofisi ya mwendesha mashtaka na vyombo vya habari wamesema.
Taarifa ya ofisi ya mwendesha mashtaka imesema jengo katika wilaya ya Hadayek al-Oubba “liliporomoka kabisa”, na kuua watu wanane.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa “wafanyakazi wa ulinzi wa raia waliwaokoa watu tisa, miongoni mwao mwanamke aliyejeruhiwa, huku wengine wanane wakiwa wamekufa.
Watu wengine watano walifanikiwa kuondoka kwenye jengo hilo kabla ya kuporomoka, taarifa hiyo imesema.
Taarifa ya ofisi ya mwendesha mashtaka imesema mwanamke huyo aliyejuriwa na wakazi wawili wametoa ushahidi “wakidokeza kuwa kuporomoka kwa jengo hilo kulisababishwa na mkazi ambaye alibomoa hivi karibuni kuta katika makazi yake kwenye ghorofa ya kwanza”, licha ya majirani kumtaka asifanye hivyo.