Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu milioni 27 wakabiliwa na uhaba wa chakula DRC

CHAKULA DRC DRC Watu milioni 27 wakabiliwa na uhaba wa chakula DRC

Fri, 8 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mafaifa (FAO) limetangaza kuwa watu wasiopungua milioni 27 hawana usalama wa chakula katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ripoti iliyotolewa na FAO kuhusu hali ya usalama wa chakula duniani imesema, Umoja wa Mataifa unatabiri kuwa hali itakuwa mbaya zaidi nchini Congo kutokana na mzozo kati ya kundi la wanamgambo wa M23 na jeshi la serikali mashariki mwa nchi hiyo.

FAO imesema mbali na machafuko ya mashariki mwa Congo DR, mgogoro wa Ukraine pia unachangia katika ukosefu mkubwa wa usalama wa chakula katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika ripoti yake, FAO imesisitiza haja ya kuzalisha chakula bora zaidi na kupunguza bei yake duniani.

Vita nchini Ukraine, janga la corona, mabadiliko ya hali ya hewa na ukame ni miongoni mwa sababu kuu zinazohatarisha usalama wa chakula duniani.

Awali taasisi kadhaa za Umoja wa Mataifa zilikuwa ziimetahadharisha kuwa, kupanda kwa bei za chakula, fueli na mbolea kote duniani kulikosababishwa na vita vya Ukraine kunaiweka dunia katika hatari ya kutumbukia kwenye mgogoro mkubwa wa chakula na baa la njaa.

Mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa likiwemo Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la Afya Duniani (WHO) yamesema kwa ujumla watu bilioni 2.3 walishuhudia uhaba wa chakula kwa kiwango cha juu na cha wastani mwaka uliopita 2021.

Mashirika hayo ya UN yamesema kupanda kwa bei ya mbolea na nishati mwaka uliopita, kumeathiri sekta ya kilimo hususan mavuno ya ngano, mchele na mahindi. Hali hiyo inahofiwa kuathiri mabilioni ya watu kote Asia, Afrika na Amerika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live