Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu milioni 25 wanateseka na njaa Sudan

WFP Inaonya Janga La Njaa Linatarajiwa Kutokea Nchini Sudan Watu milioni 25 wanateseka na njaa Sudan

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vita vya kuwania madaraka kati ya majenerali wa kijeshi vinandelea kuiangamiza Sudan huku taarifa zikisema kuwa Wasudan milioni 25 wanateseka kwa njaa kutokana na vita hivyo vya uchu wa madaraka baina ya majenerali hao wa kijeshi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Tasnim, vita kati ya jeshi SAF na vikosi vya msaada wa haraka RSF vimepamba moto katika mji mkuu wa Sudan Khartoum, huku vikosi vya RSF vikidai kuwa vimeteka maeneo na vitengo vya jeshi huko kusini na mashariki mwa Khartoum. Kwa upande wake, jeshi la Sudan limeendelea kufanya mashambulizi ya silaha nzito katika vituo vya RSF hasa kwenye maeneo ya Omdurman na al Bahri.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kikosi cha mizinga cha jeshi la Sudan kimeshambulia pia maeneo na mikusanyiko ya askari wa RSF kwenye maeneo tofauti ya Khartoum. Watu walioshuhudia wamesema kuwa wameona moshi nzito ukipanda angani baada ya kutokea mashambulizi hayo.

Vyanzo vingine vya kijeshi vimesema kuwa, jeshi la Sudan na vikosi vya kiraia vyenye silaha vimeelekea katika mji mkuu Khartoum kwenda kuongeza nguvu za wanajeshi wa SAF dhidi ya wapiganaji wa RSF. Vikosi hivyo vya jeshi la Sudan vimetokea katika mji wa Shandi, ulioko kaskazini mwa Sudan. Mamilioni ya wananchi wa Sudan wanateseka kwa njaa kali kutokana na ugomvi wa uchu wa madaraka baina ya majenerali wa kijeshi

Jenerali Abdul Fattah Burhan, mkuu wa baraza la kijeshi ambaye pia ndiye kamanda mkuu wa wa jeshi la Sudan wiki iliyopita aliamuru jeshi na makundi yote yenye silaha kushambulia vikosi vya RSF sehemu yoyote vinapokutana navyo.

Amma baya zaidi kwenye vita hivyo vya uchu wa madaraka, ni hasara na tabu wanayopata wananchi wa kawaida. Huduma za simu na Intaneti zimekatika katika maeneo mengi ya Sudan tangu Ijumaa iliyopita jioni.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao wanaiunga mkono RSF wamelilaani jeshi la Suda kwa kuripua mnara wa mawasiliano mashariki mwa Khartoum na vituo vya seva. Wanaounga mkono jeshi nao wanasema kuwa vikosi vya RSF vimeshambulia kituo kikuu cha mawasiliano cha "Sudanese" na kile cha "MTN" ndio maana mawasiliano ya simu na Intaneti yamekatika.

Zaidi ya hayo taarifa zinasema kuwa zaidi ya raia milioni 25 wa Sudan ambapo milioni 14 kati yao ni watoto wanataabika na njaa kali na wanahitaji mno misaada ya haraka ya kibinadamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live