Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu kumi wauawa katika ghasia za Amhara zilizozuka upya Ethiopia

Watu Kumi Wauawa Katika Ghasia Za Amhara Zilizozuka Upya Ethiopia Watu kumi wauawa katika ghasia za Amhara zilizozuka upya Ethiopia

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Mapigano yamepamba moto tena katika baadhi ya maeneo katika eneo lenye utulivu la Amhara nchini Ethiopia baada ya wiki moja ya utulivu, huku takriban vifo 10 vya raia vimeripotiwa.

Wakazi katika mji wa Amhara wa Debre Tabor wameambia BBC kwamba mapigano kati ya wanamgambo wa eneo hilo na wanajeshi wa serikali yalianza mwishoni mwa juma na kuendelea hadi Jumatatu asubuhi.

Kulingana na walioshuhudia, hospitali kuu ya jiji hilo ilipata uharibifu baada ya mashambulio makubwa ya risasi.

Daktari katika hospitali hiyo aliambia BBC kwamba takriban watu watano waliokuwa wakiwatembelea wagonjwa na zaidi ya raia 20, waliokuwa wakihamia karibu na kituo hicho, walijeruhiwa.

Juhudi za BBC kupata taarifa kutoka kwa mamlaka za eneo kuhusu mashambulizi haya hazijafanikiwa.

Mapigano pia yameripotiwa ndani au karibu na miji ya Debre Markos na Fenote Selam pamoja na miji midogo na vijiji katika eneo hilo.

Mvutano huko Amhara ulianza mwezi Aprili, kufuatia uamuzi wenye utata wa kufuta kikosi cha kijeshi cha kikanda.

Tangu mapema Agosti, sehemu kubwa ya eneo hili la pili kwa kuwa na watu wengi nchini Ethiopia limeshuhudia vurugu.

Wiki iliyopita baraza la eneo la Amhara lilimteua rais mpya baada ya Yilkal Kefale, ambaye aliongoza eneo hilo kwa takriban miaka miwili, kujiuzulu.

Chanzo: Bbc