Wafanyakazi wa uokoaji wanawasaka takriban watu 10, wengi wao wakiwa wajenzi, wanaohofiwa kuwa wamekwama kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.
Jengo hilo la ghorofa saba lilikuwa bado linaendelea kujengwa lilipoanguka Jumanne alasiri katika eneo la Kasarani, viungani mwa jiji.
Msimamizi anayesimamia eneo hilo mara mbili alipuuza maonyo kutoka kwa mamlaka ya kukomesha kazi ya ujenzi kufuatia wasiwasi kuhusu uthabiti wake, tovuti ya habari ya Nation inaripoti.
Kuporomoka kwa majengo yanayojengwa ni jambo la kawaida katika jiji hilo na mara nyingi husababisha vifo.
Vikosi vya dharura siku bado vipo kwenye eneo la tukio, huku mashine nzito zikisogeza vibao vya zege huku waokoaji wakijaribu kuwatafuta waliokuwa wamefukiwa kwenye vifusi.