Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu kadhaa wanahofiwa kufariki katika mlipuko wa ghala la mafuta Guinea

Watu Kadhaa Wanahofiwa Kufariki Katika Mlipuko Wa Ghala La Mafuta Guinea Watu kadhaa wanahofiwa kufariki katika mlipuko wa ghala la mafuta Guinea

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Watu kadhaa wanahofiwa kufariki na makumi ya wengine wamejeruhiwa katika mji mkuu wa Guinea, Conakry, kufuatia mlipuko katika ghala la mafuta katika kitongoji cha Kaloum.

Mlipuko huo ulitokea alfajiri ya Jumatatu - muda mfupi baada ya saa sita usiku - na uliambatana na moto, shirika la habari la AFP linaripoti.

Tovuti ya habari inayomilikiwa na watu binafsi ya Le Courrier de Conakry inaripoti kuwa takriban watu wanne wamefariki na wengine takriban 100 wamejeruhiwa katika tukio hilo.

"Ndiyo, kuna vifo na majeruhi," afisa mkuu wa polisi aliambia shirika la habari la Reuters, akiongeza kuwa bado wanahesabu. Mamlaka za kijeshi nchini humo bado hazijazungumzia tukio hilo, ikiwa ni pamoja na iwapo kuna vifo vilivyotokea.

Hospitali kuu mbili za Conakry, Ignace Deen na Donka zimejaa watu wengi waliojeruhiwa, AFP inaripoti.

Mlipuko huo ulilipua paa na madirisha kutoka kwa majengo katika eneo hilo, na kusababisha uharibifu mkubwa na kuwalazimu kadhaa kukimbia.

Kaloum ni kituo cha utawala cha Conakry ambapo ofisi ya rais na wizara nyingi zinapatikana.

Mkazi wa eneo hilo ameiambia AFP kwamba polisi wamezuia eneo la bandari na wazima moto wamejibu eneo la mlipuko.

Chanzo: Bbc