Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu kadhaa wahofuwa kufariki kwa mabomu Sudan

Kombora Nchini Sudan Lasababisha Vifo Vya Takriban Watu 22 Watu kadhaa wahofuwa kufariki kwa mabomu Sudan

Sat, 15 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miripuko miwili ya mabomu iliyotokea Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, imesababisha watu kadhaa kuuawa na kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, vyanzo vya habari nchini Somalia vilitangaza usiku wa kuamkia leo kuwa watu wanne waliuawa na wengine watano walijeruhiwa kutokana na miripuko miwili iliyotokea Mogadishu, mji mkuu wa nchi hiyo, ambayo ilisababishwa na kundi la kigaidi la Al-Shabaab.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Somalia, mripuko wa kwanza ulitokea karibu na makao makuu ya Wizara ya Ulinzi mjini Mogadishu, na mripuko wa pili ulitokana na shambulio la mtu aliyejitoa mhanga, uliolenga gari lililombeba Abdi Ahmed, naibu wa zamani wa masuala ya usalama wa gavana wa Mkoa wa Lower Shabelle, na kusababisha kifo cha afisa huyo.

Kundi la kigaidi la al-Shabaab ambalo lina mielekeo ya kifikra inayofungama na ya mtandao wa al-Qaeda, limekuwa likijaribu kuipindua serikali kuu ya Somalia tangu mwaka 2007 na limefanya operesheni nyingi za kigaidi na kuua idadi kubwa ya wanajeshi na raia.

Kundi hili la kigaidi na ukufurishaji ndilo linalohusika na miripuko mingi inayotokea nchini Somalia.

Somalia inakabiliwa pia na tishio la mabomu ya ardhini na athari za mabaki ya vita, huku Umoja wa Mataifa ukiripoti mwezi Aprili mwaka huu kwamba zaidi ya watu 1,200 wamekufa nchini humo kutokana na miripuko iliyoachwa bila kuripuka, mabomu ya kutegwa ardhini na vifurushi vya mada za miripuko.../

Chanzo: www.tanzaniaweb.live