Watu wanne wamenusuriwa baada ya daraja linajengwa kutoka uwanja wa Ndege wa JKIA kuelekea Westlands kuporomoka eneo la Kangemi siku ya Jumatatu, Juni 21 jioni.
Wafanyakazi wengine wawili wa kampuni hiyo ya Uchina waliokuwa wakijenga daraja hilo waliachwa na majeraha mabaya na walikimbizwa katika hospitali kwa ajili ya kupokea matibabu.
Aidha, watu kadhaa wanahofia kupoteza maisha yao baada ya kufunikwa kwenye vifusi, afisa mkuu wa polisi kata ndogo ya Westlands Lilian Obura amethibitisha kwamba shughuli ya uokoaji inaendelea.
Hata hivyo, idadi ya waliokwama kwenye vifusi bado haijabainika.
Kulingana na shahidi, baadhi ya mafundi walifunikwa kwenye vifusi baada ya nguzo za daraja hilo kuporomoka.
Maafisa wa polisi wanachunguza chanzo cha mkasa huo huku hofu ya waliokwama kwenye vifusi ikishamiri kwenye mitandao ya kijamii.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 073248269.
Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka TUKO hapa