Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 92 wamefariki Madagascar

Vurugu Madagascar.jpeg Watu 92 wamefariki Madagascar

Sat, 26 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa kutoka Antananarivo, mji mkuu wa Madagascar zinasema kuwa watu wasiopungua 12 wamepoteza maisha na karibu 80 wengine wamejeruhiwa baada ya kutokea mkanyagano Ijumaa jioni kwenye lango la uwanja wa michezo wa Barea wa mjini humo.

Waziri Mkuu wa Madagascar, Christian Ntsay amethibitisha habari hiyo ya kupoteza maisha na kujeruhiwa watu 92 kwenye lango la uwanja huo wa michezo wa Barea katika mji mkuu Antananarivo na kuongeza kuwa, msongamano huo ulitokea kabla ya sherehe za ufunguzi wa Michezo ya 11 ya ukanda wa Bahari ya Hindi.

Amesema hayo mbele ya vyombo vya habari na kuongeza kuwa: "Kwa sasa, idadi ya waliofariki ni 12 na karibu 80 wamejeruhiwa, na 11 kati yao wanahitaji upasuaji wa haraka."

Waziri Mkkuu wa Madagascar pia amesema: "Jimbo (la Barea) linagharamia matibabu ya majeruhi na kwa niaba ya taasisi zote za serikali, natoa pole kwa familia za wahanga."

Pamoja na hayo, sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo zimefanyika kama kawaida, lakini wakati wa sherehe hizo, Rais Andry Rajoelina aliongoza kimya cha dakika moja cha kuwasikitikia waathiriwa wa mkanyagano na msongamano huo.

Mara kwa mara Madagascar huwa inakumbwa na matukio kama hayo, mafuriko, vimbunga na ajali zinayochukua roho za watu wengi. Mwezi Januari mwaka huu, watu 30 wapoteza maisha kutokana na kimbunga cha tropiki nchini humo.

Mwezi Machi mwaka huu pia, watu 22 walikufa maji na 32 miili yao haikupatikana katika ajali za boti huko Madagascar.

Mwezi Februari mwaka jana pia, watu 120 walifariki dunia kwa kimbunga cha Batsirai katika kisiwa hicho kikubwa zaidi barani Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live