Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 91 wafariki katika ajali ya meli Msumbiji

Msumbiji Watu 91 wafariki katika ajali ya meli Msumbiji

Mon, 8 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban watu 91 wamepoteza maisha baada ya boti iliyokuwa imejazwa mizigo kupita kiasi kupinduka na kuzama karibu na Kisiwa cha Msumbiji katika jimbo la kaskazini mwa Msumbiji la Nampula siku ya Jumapili.

Wahasiriwa waliouawa ni pamoja na watoto, na watu wengine 34 hawakupatikana, ripoti imesema, ikiongeza kuwa manusura watano wamepatikana.

Meli hiyo ilikuwa ikitokea wilaya ya Mossuril na kubeba jumla ya abiria 130, mkuu wa Jimbo la Nampula Jaime Neto, amenukuliwa akisema.

Neto amesema kwamba abiria walikuwa wamekimbia makazi yao kufuatia hofu iliyosababishwa na habari potofu kuhusu mlipuko wa kipindupindu.

Neto amesema "Ni meli ambayo haijatayarishwa kusafirisha watu wengi. Ni meli ya uvuvi, na watu walikuwa na taarifa potofu kuhusu mlipuko wa kipindupindu, na wakakimbilia kwenye chombo."

Jitihada zinaendelea kuwatafuta waliotoweka na kufanya uchunguzi wa ajali hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live