Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 80 wauawa katika shambulio langa Nigeria

Shambulii Anga Nigeria.jpeg Watu 80 wauawa katika shambulio langa Nigeria

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban raia 80 Waislamu wameuawa katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria kufuatia mashambulizi ya anga ya jeshi la Nigeria.

Wakati jeshi la Nigeria linadai kuwa waliouawa ni majambazi na watu wanaojihusisha na vitendo vya kigaidi, baadhi ya duru zinapinga madai hayo ni kusema waliouawa ni raia wa kawaida.

Taarifa ya jeshi la Nigeria imesisitiza kuwa, imefanya operesheni kubwa ya kijeshi katika maeneo yanayosadikiwa kuwa ni ngome za magaidi na wahalifu sugu.

Tukio hilo linajiri siku mbili tu baada ya jeshi la Nigeria kutangaza kuwa, limeua zaidi ya magaidi 180 wanaoaminika kuendesha mashambulizi ya kigaidi katika kona mbalimbali za nchi hiyo.

Edward Buba, Msemaji Taifa wa Jeshi la Nigeria, aliwaambia waandishi wa habari katika mji mkuu wa nchi hiyo Abuja kwamba takriban watu wengine 204 wamekamatwa na mateka 234 wamekombolewa kwenye operesheni za jeshi hilo.

Wanamgambo wa Boko Haram wa Nigeria wamekuwa wakitekeleza mashambulio ya kigaidi katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika

Mashambulizi ya kutumia silaha yamekuwa tishio kubwa la usalama katika mikoa ya kaskazini na katikati mwa Nigeria. Mashambulio hayo yamesababisha vifo na utekaji nyara wa watu wengi wasio na hatia katika miezi ya hivi karibuni.

Mwanzoni mwa mwezi ulioisha wa Novemba, maafisa wa polisi ya Nigeria walitangaza kwamba katika siku za hivi karibuni raia wasiopungua 40 wameuawa katika shambulio la magaidi wa Boko Haram kwenye jimbo la Yobe la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu pia, Jeshi la Nigeria liiliitangaza kuwa,, magaidi 31 wenye silaha wameangamizwa na wanajeshi wa Nigeria katika operesheni mbalimbali zilizofanywa na jeshi hilo katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika kwenye kipindi cha wiki moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live