Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 8 wauawa wakisherehekea siku ya kuzaliwa Afrika Kusini

Afrika Kusini Pic Watu 8 wauawa wakisherehekea siku ya kuzaliwa Afrika Kusini

Mon, 30 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wenye silaha walifyatulia risasi kundi la watu waliokuwa wakisherehekea siku ya kuzaliwa mwishoni mwa juma katika kitongoji kimoja nchini Afrika Kusini, na kuwauwa watu nane na kuwajeruhi wengine watatu, polisi nchini humo wamesema leo Jumatatu.

Msherehekeaji wa siku ya kuzaliwa ni miongoni mwa waliouawa kwa kupigwa risasi katika mji wa Gqeberha, ambao zamani ulikuwa ukiitwa Port Elizabeth.

"Mmiliki wa nyumba hiyo alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa wakati watu wawili wasiojulikana wenye bunduki waliingia ndani Jumapili jioni na kuanza kuwafyatulia risasi wageni," polisi wamesema katika taarifa yao.

“Watu wenye silaha waliwafyatulia risasi wageni. Watu wanane wamefariki huku wengine watatu wakiendelea kutibiwa hospitalini. Mwenye nyumba ni miongoni mwa waliofariki," imesema taarifa ya polisi.

Kwa mujibu wa VOA, Nomthetheleli Mene, Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Eastern Cape, amelaani mauaji hayo ambayo ameyaita ni ukatili wa kibinadamu.

Uchunguzi umeanzishwa kuhusu shambulio hilo na polisi wamesema msako wa kuwasaka wahusika unaendelea.

Mwaka jana Afrika Kusini ilishuhudia mfululizo wa matukio ya ufyatuaji risasi na kuua makumi katika baa tofauti katika vitongoji vya wafanyakazi huko Johannesburg na katika Jiji la mashariki la Pietermaritzburg.

Waziri wa Polisi Bheki Cele, Kamishna wa Polisi wa nchini humo, Fannie Masemola na wataalamu wa uhalifu wamekwenda eneo la shambulio ili kubaini madhara zaidi yaliyojitokeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live